Description
Kama mwajiriwa, una ndoto ya kuwa na biashara yako, lakini huna muda, huna mtaji mkubwa, na unaogopa kuacha kazi? Kitabu *BIASHARA 50 BORA KWA WAAJIRIWA* ndio mwongozo uliokuwa unamtafuta.Hiki si kitabu cha hadithi za kutajirika haraka. Hiki ni kitabu cha vitendo.* *Utapata nini ndani?* *SURA YA 1: Kanuni 7 za Dhahabu* Jinsi ya kuanzisha biashara bila kugombana na mwajiri wako, kutenga pesa, na kujua faida halisi. *SURA YA 2: Biashara 50 Zilizogawanywa Makundi* Kila biashara nimekuwekea: - Mtaji wa kuanzia kwa TZS (kuanzia 80,000 tu) - Jinsi ya kuanza ukiwa kazini - hatua kwa hatua - Cha kuzingatia ili usiingie hasara Kutoka: Uuzaji wa nguo WhatsApp, printing shuleni, kuku wa mayai, bodaboda, UTT na Hisa DSE, hadi TikTok ya elimu na kukodisha viti! *SURA YA 3-6: Mpango wa Siku 30* Jinsi ya kuchagua wazo 1 linalokufaa, bajeti, na fomu za kurekodi mauzo. *Kitabu hiki ni kwa nani?* - Mwalimu anayetaka kipato cha ziada - Mwajiriwa anayetaka kuanzisha side hustle - Kijana anayetaka kuwekeza mshahara wake kwa akili *Mwandishi: Selapion Mfuse* Mwalimu, mwekezaji wa DSE na UTT.