Sera na Masharti ya Watoa Huduma
Masharti haya yanahusu huduma ya Watoa Huduma ya Bongofey, inayoendeshwa na Bongofey Limited. Yanaongezea Masharti ya Matumizi, Sera ya Faragha na Kanusho ya Bongofey.
Kwa ufupi
- Bongofey inawaunganisha wateja na watoa huduma huru. Sisi si waajiri, mawakala wala wadhamini wao.
- Ada ya TZS 1,000 ni ya kuona namba ya simu na WhatsApp, si malipo ya kazi. Bei ya kazi mnakubaliana wenyewe.
- Alama ya Blue, Green au Gold inaonyesha mtoa huduma amejiunga na kifurushi cha Bongofey. Si uthibitisho wa ujuzi, leseni au tabia.
- Usilipe kazi kabla ya kumwona mtoa huduma au kazi yenyewe. Kwa dharura piga 112.
- Wasifu ulioongezwa na Bongofey unaweza kudaiwa na mhusika, au kuondolewa akiomba.
In English: Bongofey only connects customers with independent service providers. The viewing fee pays for contact details, not for the work. Badges are paid packages, not a check of skills, licences or background. Agree the price before any work and never pay in advance to someone you have not met.
1. Bongofey ni jukwaa la kuunganisha
Watoa huduma wanaoonekana kwenye Bongofey (mafundi, madaktari, walimu, madereva, wauza maji na wengine) ni watu au biashara huru. Wao ndio wanaowajibika kwa taarifa zao, bei, ubora, usalama na uhalali wa huduma wanazotoa. Makubaliano yoyote ya kazi ni kati ya mteja na mtoa huduma. Bongofey haishiriki kwenye makubaliano hayo, haipokei malipo ya kazi, na haiwezi kudai au kurejesha pesa za kazi kwa niaba ya mtu yeyote.
2. Kwa wateja
- Ada ya kuona namba. Unalipa TZS 1,000 kwa simu ili kuona namba ya simu na WhatsApp ya mtoa huduma mmoja. Namba inabaki wazi kwako kwa siku 30 kwenye kifaa ulichotumia kulipa.
- Marejesho. Ada hairudishwi kwa sababu mtoa huduma hakupokea simu, hakupatikana kwa siku hiyo, au hamkukubaliana bei. Kama namba haifanyi kazi kabisa au si ya mtu huyo, tuambie au tumia kitufe cha "Ripoti" ndani ya siku 7. Tutachunguza, na tukithibitisha tatizo tunaweza kukurudishia ada au kukufungulia mtoa huduma mwingine bila malipo.
- Usalama. Kubaliana bei na kazi kwa maandishi (SMS au WhatsApp). Usitume malipo ya awali kwa mtu ambaye hujamwona. Kwa huduma za afya, sheria au umeme, muulize mtoa huduma leseni yake. Kwa dharura, piga 112.
- Maoni. Mtu yeyote aliyepata huduma anaweza kuandika maoni. Maoni ya waliolipia kuona namba kupitia Bongofey yanaonyesha alama ya "Amewasiliana kupitia Bongofey". Andika ukweli kuhusu huduma uliyopata. Usiandike matusi, taarifa binafsi za mtu, wala maoni ya kulipwa. Tunaweza kuficha maoni ya uongo au yasiyofaa.
3. Kwa watoa huduma
- Taarifa zako (jina, kazi, maeneo, namba, maelezo) lazima ziwe za kweli na za sasa. Picha unazoweka lazima ziwe zako au uwe na ruhusa ya kuzitumia.
- Kama kazi yako inahitaji leseni au usajili kisheria (mf. afya, sheria, uhandisi au ufungaji wa umeme), lazima uwe nayo halali. Bongofey inaweza kukuomba uthibitisho.
- Haruhusiwi: huduma zilizokatazwa na sheria, udanganyifu, kudai malipo ya awali bila nia ya kufanya kazi, kutumia wasifu wa mtu mwingine, maoni ya kujiandikia, au maudhui ya chuki na ya kingono.
- Tunaweza kuficha, kusimamisha au kufuta wasifu unaovunja masharti haya au unaolalamikiwa, na tunaweza kufanya hivyo bila taarifa ya awali pale usalama wa wateja unapohusika.
- Una wajibu wa kodi na vibali vya biashara yako. Bongofey haikulipi mshahara wala haikuajiri.
4. Alama za uthibitisho na Boost
- Blue Verified, Green Verified na Gold Verified ni vifurushi vya kulipia vinavyompa mtoa huduma alama na nafasi ya juu zaidi kwenye orodha. Alama inaonyesha amejiunga na kifurushi. Haimaanishi Bongofey imekagua ujuzi, vyeti, leseni au historia yake, isipokuwa tutakaposema hivyo waziwazi kwenye wasifu husika.
- Boost inamweka mtoa huduma juu ya orodha, kwenye ukurasa wa mwanzo na kwenye matangazo ya Bongofey kwa muda wa kifurushi. Haihakikishi idadi fulani ya wateja au simu.
- Malipo ya vifurushi hayarudishwi. Ukinunua kifurushi kingine kabla ya cha sasa kuisha, siku zilizobaki zinaongezwa. Wasifu ukisimamishwa kwa kuvunja masharti, siku zilizobaki hazirudishwi.
5. Wasifu ulioongezwa na Bongofey (kudai au kuondoa)
Bongofey inaweza kuongeza wasifu wa mtoa huduma aliyekubali, au kwa taarifa alizotupa yeye au biashara yake. Mhusika anaweza:
- Kuudai kwa kubofya "Udai" kwenye wasifu, kujisajili kama Mtoa Huduma na kuthibitisha namba iliyo kwenye wasifu (kwa code ya SMS au kwa admin kumpigia simu). Baada ya hapo anaweza kubadilisha taarifa zote.
- Kuomba uondolewe wakati wowote kupitia Wasiliana Nasi. Tutaondoa wasifu haraka iwezekanavyo baada ya kuthibitisha kuwa ombi limetoka kwa mhusika.
6. Faragha: taarifa tunazokusanya na tunavyozitumia
- Watoa huduma. Jina, kazi, maeneo, maelezo, picha na maoni ya wateja vinaonekana kwa umma na vinaweza kuonekana kwenye Google. Namba ya simu na WhatsApp zinaonyeshwa kwa waliolipia ada ya kuona namba pekee. Barua pepe ya akaunti haionyeshwi.
- Wateja. Tunahifadhi namba uliyolipia nayo pamoja na rekodi ya malipo, na kitambulisho cha kivinjari (cookie) kinachokumbuka namba ulizolipia. Ukiandika maoni tunahifadhi jina ulilotumia, maoni yako na anwani ya IP (kuzuia maoni ya uongo). Ukiripoti wasifu tunahifadhi anwani ya IP ili kuzuia matumizi mabaya.
- Matumizi. Tunatumia taarifa hizi kuendesha huduma, kuthibitisha malipo, kuzuia udanganyifu na kujibu malalamiko. Hatuuzi taarifa zako. Tunazishiriki tu na watoa huduma wa malipo (BongoPay na mitandao ya simu) na wa SMS pale inapohitajika kukamilisha huduma.
- Mtoa huduma hapati namba yako unapolipia kuona namba yake. Atajua umewasiliana naye pale tu utakapompigia au kumtumia ujumbe.
- Haki zako. Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Tanzania ya mwaka 2022, unaweza kuomba kuona, kurekebisha au kufuta taarifa zako kupitia Wasiliana Nasi. Rekodi za malipo tunaweza kuzihifadhi kwa muda unaotakiwa na sheria za kodi na hesabu.
7. Kanusho
Bongofey haitoi dhamana yoyote kuhusu ubora, usalama, uhalali, upatikanaji au bei ya huduma zinazotolewa na watoa huduma, wala kuhusu ukweli wa taarifa walizoweka. Kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria za Tanzania, Bongofey haitawajibika kwa hasara, majeraha, uharibifu wa mali au migogoro inayotokana na huduma iliyotolewa na mtoa huduma aliyepatikana kupitia jukwaa hili. Maelezo ya watoa huduma wa afya au sheria ni taarifa zao binafsi, si ushauri wa kitaalamu kutoka Bongofey.
8. Mabadiliko na mawasiliano
Tunaweza kubadilisha masharti haya. Mabadiliko yanaanza kutumika yanapowekwa kwenye ukurasa huu. Kuendelea kutumia Watoa Huduma baada ya mabadiliko kunamaanisha unayakubali. Masharti haya yanaongozwa na sheria za Tanzania.
Maswali, malalamiko au ombi la kuondolewa? Wasiliana Nasi.