Description
Waajiri wengi siku hizi hawaangalii CV pekee — wanakutafuta pia LinkedIn kabla ya hata kukuita usailini. Kitabu hiki kinakuonyesha jinsi ya kujenga profaili yenye mvuto hatua kwa hatua: kuchagua picha na jalada linalofaa, kuandika Headline inayovutia macho, kujaza sehemu ya "Kuhusu" kwa mtindo wa kibinadamu, kuonyesha uzoefu wako wa kazi na elimu kwa usahihi, kuchagua ujuzi unaovutia zaidi, kujenga mtandao wa wataalamu, na kutumia maneno muhimu (keywords) yanayotafutwa na waajiri. Kinajumuisha pia makosa ya kawaida yanayofanya profaili zisionekane kwenye utafutaji wa waajiri. Kinafaa kwa wahitimu wapya na mtu yeyote anayetaka kujenga uwepo wa kitaaluma mtandaoni.