Description
Je, umewahi kujikuta ukijisahau kwa ajili ya kuwafurahisha wengine? Umewahi kuhisi ndoto zako zinapotea kwa sababu ya changamoto za maisha, mahusiano au maneno ya watu? Kitabu hiki kimeandaliwa kwa ajili yako. Jipende, Jithamini na Jitambue ni kitabu kinachomsaidia mwanamke kuelewa thamani yake, kujenga upendo binafsi, kujiamini na kutambua kuwa bado ana nafasi ya kutimiza ndoto zake. Kupitia kitabu hiki utajifunza: • Jinsi ya kujitambua na kutambua thamani yako. • Kujipenda bila kujilinganisha na wengine. • Kutokuzika ndoto zako kwa sababu ya changamoto. • Kuanza kujenga maisha unayoyatamani. • Kuwa mwanamke mwenye malengo na msimamo. Kumbuka, thamani yako haipimwi kwa namna watu wanavyokuona. THAMANI YANGU Jitambue. Jithamini. Jenga maisha unayoyatamani.