Description
JOKAZA ni riwaya inayosimulia maisha ya kijana wa miaka 20 kutoka Arusha, Tanzania, anayepitia umasikini mkubwa baada ya kufiwa na wazazi wake na kubaki na mdogo wake SOLIA, mwenye miaka 12. Akiwa ameachia shule Kidato cha Tatu, Jokaza anapambana kutafuta kazi, chakula na maisha bora huku akimlea mdogo wake katika mazingira magumu. Maisha yao yanabadilika baada ya kukutana na MR. ENOCK, Mjerumani mwenye miaka 65 na mwekezaji wa hoteli Tanzania. Lakini furaha ya kupata kazi inakatizwa na kifo cha Solia kutokana na ugonjwa wa Sickle Cell. Akiwa amevunjika moyo na kubaki mpweke, Jokaza anapata msaada, malezi, elimu na mafunzo kutoka kwa Mr. Enock, na kuanza safari mpya ya kujijenga, mafanikio na mapenzi. Ni hadithi ya maumivu, udugu, upotevu, uvumilivu na matumaini inayothibitisha kuwa mazingira magumu si mwisho wa maisha.