Afisa Lishe - Peter Tangasi
Kuhusu Afisa Lishe - Peter Tangasi
Mimi ni Afisa Lishe mwenye taaluma ya Sayansi ya Chakula na Teknolojia. Natoa elimu na miongozo ya lishe inayolenga kusaidia watu kuboresha afya zao, kuzuia changamoto zinazohusiana na ulaji na kujenga maisha yenye afya bora.
Kupitia eBooks na miongozo yangu, ninakusaidia kuelewa na kutumia lishe katika maeneo mbalimbali ya afya, yakiwemo:
✓Kupunguza uzito na kitambi: Mbinu za kupunguza mafuta mwilini kwa kutumia vyakula vya kawaida.
✓Afya ya uzazi: Elimu ya lishe kwa wanaume na wanawake, afya ya mbegu za kiume, afya ya mfumo wa uzazi na maandalizi ya ujauzito.
✓Lishe ya mama na mtoto: Lishe wakati wa ujauzito, kunyonyesha na ukuaji wa mtoto.
✓Magonjwa yasiyoambukiza: Lishe kwa watu wenye kisukari, shinikizo la damu na changamoto nyingine za kiafya.
✓Lishe ya kila siku: Jinsi ya kula vizuri, kwa gharama nafuu na kulingana na mahitaji ya mwili.
Lengo langu ni kubadilisha maarifa ya lishe kuwa vitendo vinavyoweza kuboresha maisha yako.
Afya bora inaanzia kwenye sahani yako. Jifunze kula vizuri, linda afya yako na wekeza kwenye maisha yako!